Mechi namba 28 Kundi B (Kilimanjaro Heroes 0 v Pepsi
2). Klabu ya Kilimanjaro Heroes imepigwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili)
kwa kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) katika mechi
hiyo iliyofanyika Februari 3, 2018 katika Uwanja wa Ushirika mjini Moshi,
kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Taratibu za Mchezo.
Adhabu dhidi ya Kilimanjaro Heroes imetolewa kwa kuzingatia
Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mechi namba
30 Kundi B (African Sports 2 v AFC 0). Wachezaji wa AFC, John George Rasta
na Shaibu Salim wanapelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kutaka kumshambulia
Mwamuzi kabla ya kuokolewa na viongozi wa timu hiyo katika mechi hiyo
iliyofanyika Februari 3, 2018 katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Klabu ya AFC
imepigwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa kutoingia vyumbani wakati wa
mapumziko, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(13) ya Ligi Daraja la
Pili kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya
14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
No comments:
Post a Comment