Mechi namba 122 (Lipuli 0 vs Yanga 2). Klabu za Lipuli
na Yanga kila moja imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kutumia
milango isiyo rasmi kuingia uwanjani, kitendo ambacho ni ukiukaji wa Kanuni ya
14(14) ya Ligi Kuu. Adhabu dhidi yao imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49)
ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Pia klabu ya
Yanga imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kutoingia vyumbani, hivyo
kwenda kinyume na Kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za
Mchezo.
Mechi namba
123 (Singida United 3 vs Mwadui 2). Kocha wa makipa wa Mwadui, Lucheke
Gaga amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya
kuondolewa kwenye benchi (ordered off) na Mwamuzi kwa kutoa lugha ya matusi
katika mechi hiyo iliyofanyika Februari 3, 2018 kwenye Uwanja wa Namfua mjini
Singida. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 40(11) ya Ligi Kuu
kuhusu Udhibiti wa Makocha.
Mechi namba
128 (Ruvu Shooting 0 vs Simba 4). Mchezaji wa Ruvu Shooting, Mau Bofu
amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kumpiga
kiwiko Emmanuel Okwi wa Simba katika mechi hiyo iliyofanyika Februari 4, 2018
kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya
37(3) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.
No comments:
Post a Comment