WAAMUZI waliochezesha
mchezo wa Ligi daraja la kwanza dhidi ya Dodoma FC na Alliance Schools
uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma, Desemba 30, 2017 wamefungiwa miaka
mitatu kila mmoja kwa kuzingatia Kanuni ya 38(1a) ya Ligi Daraja la Kwanza
kuhusu udhibiti wa waamuzi.
Akizungumza leo Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB) Boniface Wambura alisema pamoja na
kufungiwa waamuzi hao Kamati ya saa 72 imeomba suala la waamuzi hao ambao
baadhi yao ni wa Ligi Kuu, kupitia TFF liwasilishwe kwenye chombo chenye
dhamana ya kisheria ya rushwa kufanyiwa uchunguzi zaidi.
“Waamuzi hao
ni Andrew Shamba, Abdallah Mkomwa, Athuman Athuman na Omari Juma kwa kuchezesha
mechi hiyo chini ya kiwango na Kamishna wa mechi hiyo Mackshem T. Nzunda kwa
kushindwa kutoa taarifa ya mchezo kwa usahihi,” alisema Wambura
Pia Wambura
alisema kamati imetupa malalamiko ya Alliance Schools kupinga uchezeshaji wa
mwamuzi wa Andrew Shamba katika mchezo huo kwa vile hayakuwa na vielelezo wala
kanuni za kuyathibitisha kwani suala la kutunza muda ni kazi ya mwamuzi.
Aidha
mchezaji Shaban William wa Alliance Schools amesimamishwa, hadi suala lake la
kumpiga mwamuzi litakaposikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF na timu hiyo
imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa timu hiyo kuonyeshwa kadi zaidi ya tano
katika mechi hiyo.
Klabu ya
Mufindi United, Mawenzi Market, Mkamba Rangers, Kitayosce zimepigwa faini ya
sh. 500,000 kila moja, kocha wa Green Warriors, Azish Kondo amefungiwa mechi
tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000 huku timu ya Nyanza FC ikishushwa madaraja
mawili na kutozwa faini y ash 2,000,000
No comments:
Post a Comment