MSHAMBULIAJI
wa Yanga, Obrey Chirwa na Lambart Sabiyanka wa Tanzania Prisons wamesimamishwa
kutokana na kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu hadi malalamiko dhidi yao yatakaposikilizwa
na Kamati ya Nidhamu ya TFF.
Akizungumza
jana Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB) Boniface Wambura alisema kamati ya
saa 72 ilikutana juzi na kupitia taarifa mbalimbali za ligi na kuzitolea maamuzi.
“Kamati
imeiomba TFF iipatie Bodi ya Ligi uamuzi
wa Kamati ya Nidhamu juu ya mchezaji wa Yanga kusimamishwa baada ya
mechi dhidi ya Mbao FC wakati akisubiri mashtaka yake ili kuufanyia kazi kwa
ajili ya mapendekezo ya marekebisho ya Kanuni,” alisema Wambura.
Tanzania
Prisons, Ndanda FC, Mwadui FC, Mbao FC Zimepigwa faini ya sh 500,000 kila moja
kutokana na makosa mbalimbali kwa kuzingatia kanuni za ligi kuu pia Mbao FC,
Etiene Ndayiragije amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000.
Pia
Mtunza Vifaa wa Lipuli
FC, George Mketo amesimamishwa akisubiri suala lake la kuwatukana waamuzi na
Kamishna Billy Mwilima amepewa onyo kali kwa kuruhusu mchezaji Hamisi Msabila
wa Mbeya City kucheza mechi bila kuonyesha leseni
Aidha Kamati
imeiomba Sekretarieti ya Bodi ya Ligi kutoa Waraka mwingine kwa klabu
kuzikumbusha kuhusu kutoa orodha ya wachezaji kwenye kikao cha maandalizi ya
mechi.
No comments:
Post a Comment