TANZANIA inatarajiwa
kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA)
utakaofanyika Februari 22, 2018 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere Dar es Salaam.
Mkutano huo
utashirikisha mataifa 19 ambao ni wanachama wa FIFA na Mwenyekiti wa mkutano
akiwa anatarajiwa kuwa Rais wa FIFA Gianni Infantino
Akizungumza
na wandishi wa habari jana Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace
Karia ni heshima kwa Tanzania na TFF kuwa mwenyeji wa mkutano huo mkubwa na
kuwaomba wadau mbalimbali kutumia fursa hiyo kutangaza vivutio vilivyopo nchini.
“Tunamshukuru
Mungu kupata fursa hii ya kuwa mwenyeji na ni faraja kubwa kwetu na nchini kupata
nafasi hii kwani inaonyesha ni jinsi gani tulivyo wasafi,” alisema Karia.
Karia
alisema FIFA haiwezi kupeleka mkutano mkubwa kama huu bali kuna kitu wamekiona
hivyo anashukuru uongozi wa nchi kwa namna wanavyoongoza kwa kufuata utawala
bora
Pia Karia
alisema miongoni mwa agenda zitakazojadiliwa ni pamoja na utoaji wa fedha za
FIFA kwa ajili ya maendeleo ya soka, changamoto za usajili kwa njia ya mtandao
Transfer Matching System (TMS).
Mataifa mengine
yatakayoshiriki mkutano huo ni Algeria, Mali, Morocco, Burkinafaso, Angola,
Niger, Bahrain, Palestina na Saud Arabia.
Mengine ni
Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ivory Coast, Tunisia, Bermuda, Monserrat,
St Lucia, Visiwa vya US Virgin, Maldives na Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo.
No comments:
Post a Comment