WAKATI Simba
ikishuka dimbani kesho, mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi ameomba radhi wachezaji
wenzake, viongozi na benchi la ufundi baada ya kukosekana kwenye kikosi kwa
muda mrefu bila sababu za msingi.
Simba kesho inashuka dimbani jijini Dar es Salaam kucheza dhidi ya Singida United katika
mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza Kocha wa Simba, Masoud Djuma alisema amemsamehe Emmanuel Okwi, kwani
aliomba radhi kwake, kwa uongozi na wachezaji wenzake na juzi alianza rasmi
mazoezi na timu.
“Unajua
binadamu hakuna aliyekamilika cha lazima ni muunganiko wa pamoja, tukianza
kunyoosheana vidole nguvu inapungua cha lazima ni kurudisha nidhamu kwenye
timu. Hakuna mchezaji au mtu yeyote ambaye yuko juu ya timu, hata rais wa timu
hayuko juu ya timu, timu inakuja kwanza halafu mtu baadaye,” alisema Masoud.
Pia Masoud
amemuombea radhi Emmanuel Okwi kwa mashabiki, akiwataka kuungana ili timu
ifanye vizuri katika mchezo wa leo dhidi ya Singida United na michezo ijayo.
Simba ambayo
ilikuwa imeweka kambi mkoani Morogoro ilirejea Dar es Salaam kwa ajili ya
mchezo wa leo dhidi Singida United utakaochezwa kwenye wa Taifa.
Mchezo huo
unachezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam baada ya serikali kuruhusu
kutumika kwa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara na zile za kimataifa zilizo chini
ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).
Baada ya
mchezo leo, Yanga watautumia Jumapili watakapokabiliana na Ruvu Shooting, kwani
umeruhusiwa kutumika mara moja pekee kwa wiki.
Serikali
iliufungia uwanja huo tangu Septemba mwaka jana kwa ajili ya matengenezo ambayo
tayari yamekamilika.
No comments:
Post a Comment