Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, October 8, 2017

TAIFA STARS ILIVYOPIGANA MBELE YA WATANZANIA JANA







TAIFA Stars jana ilitoka sare ya bao 1-1 na Malawi ‘The Flames’ katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku Kocha Mkuu, Salum Mayanga akilia na mwamuzi Israel Nkongo kwamba hakuitendea haki timu yake.

Mayanga akizungumza baada ya mchezo huo, alisema vijana wake walicheza vizuri, lakini baadhi ya matukio yaliyokuwa yakiamriwa na Nkongo hayakuwa mazuri kwa Stars na kwamba hakuchezesha vizuri.

Katika mchezo huo Stars ilimaliza ikiwa na wacheza pungufu uwanjani, baada ya beki Erasto Nyoni na kiungo Muzamiru Yassin kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa nyakati tofauti kipindi cha pili.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na Nkongo aliyesaidiwa na Frank Komba na Soud Lila wote waaamuzi wenye beji ya Fifa na raia wa Tanzania, mashabiki walishuhudia Malawi ikienda mapumziko ikiwa na bao 1-0 lililofungwa na Robert Ng’ambi dakika ya 35 kwa kichwa akitumia vyema makosa ya mabeki wa Stars.

Washambuliaji wa Taifa Stars wakiongozwa na nahodha Mbwana Samatta na Simon Msuva walipata nafasi kadhaa za kufunga, lakini umaliziaji haukuwa mzuri. Bao la Stars lilifungwa na Msuva dakika ya 57.

Dakika ya 75 mwamuzi Nkongo alimpandisha jukwaani Kocha Mkuu wa Malawi, Ron van Geneugden kutokana na utovu wa nidhamu, kabla ya Nyoni kuoneshwa kadi nyekundu baada ya kumpiga mchezaji wa Malawi, Mbulu Richard. Kabla ya dakika ya 89 Muzamiru kuoneshwa kadi ya pili ya njano iliyofuatiwa na nyekunu kwa kosa la mchezo mbaya.


Stars:  Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Abdi Banda, Kevin Yondan, Himid Mao, Simon Msuva/Adul Hilal, Hamisi Abdallah/Muzamiru Yassin, Mbwana Samatta, Raphael Daudi/Mbaraka Yussuf na Shiza Kichuya/Ibrahim Ajibu.

No comments:

Post a Comment