Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, October 8, 2017

SIMBA KUOGA MAHELA KABLA YA KUIVAA YANGA KATIKA MCHEZO WA LIGI

Image result for MO DEWJI
MAMBO yanazidi kunoga kuelekea mchakato wa mabadiliko ya klabu ya na sasa wale wanaotaka kuwekeza kwenye klabu hiyo wajipange na mwisho wa kutuma maombi ya kuimiliki Simba ni Oktoba 18 mwaka huu.
Hiyo maana yake itakuwa ni siku kumi kabla ya Simba kuivaa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Jana Mwenyekiti wa Kamati ya Zabuni ya Simba, Jaji mstaafu, Jaji Thomas Mihayo alisema taarifa rasmi ya mwaliko wa kuchukua nyaraka utatangazwa  katika vyombo vya habari kwa muda wa siku 10.
“Wazabuni  wanatakiwa kujiandaa na kuwa na nyaraka muhimu na kufanya mashauriano kabla ya kuwasilisha nia ya kushiriki mchakato  wa kiuwekezaji ambao utafungwa Oktoba 18,” alisema Jaji Mihayo.
Pia alisema baadae itafuatiwa na uchambuzi wa mawasilisho yatakayopokelewa, ili kutambua wazabuni  watakaokuwa wamekidhi sifa  na vigezo.
Pia Jaji Mihayo alisema jopo la wathamini  wenye sifa  na uzoefu limeundwa, ili kupitia maombi yote yatakayopokelewa, baada ya kukamilisha tathmini na wazabuni  watakaokuwa wamekidhi sifa na vigezo watapokea nyaraka za zabuni kwa ajili ya kuendelea na hatua zinazofuata.
Alisema kamati itaendelea kutoa taarifa kuhusu hatua zitakazofuata  kadri itakavyohitajika, ili kuhakikisha wanachama, mashabiki, wadau  na taasisi zenye mamlaka ya kimichezo na usimamizi zinapata fursa ya kufuatilia mchakato huo.
Agosti 20, mwaka huu, wanachama 1,216 wa klabu ya Simba waliridhia mfumo wa klabu yao kuuza Hisa baada ya Mkutano uliofanyika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere (MNICC), Dar es Salaam.

Katika mkutano huo, Kaimu Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Salim Abdallah 'Try Again' alisema asilimia 50 ya hisa zitauzwa kwa mwekezaji yeyote au wowote watakaoungana wasiozidi watatu, kwa sharti moja tu la kuwa wanachama wa klabu hiyo. 

Alisema mwekezaji anatakiwa kuweka dau lisilopungua Sh. Bilioni 20, ili kupatiwa asilimia 50 ya hisa za klabu, wakati kwa kuanzia wanachama wote wa Simba wamepewa asilimia 10 ya hisa.
Alisema asilimia nyingine 40 zitawekwa kama mtaji wa klabu na zitauzwa kwa wanachama baadaye, lakini wale wawekezaji walionunua asilimia 50 awali, hawataruhusiwa kununua hata hisa moja kwenye asilimia 40 za mtaji.

No comments:

Post a Comment