WAZIRI wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ameiomba kampuni ya
Maltchoice Tanzania kumshika mkono katika maandalizi ya pambano la Bondia
Ibrahim Class anayetarajiwa kupanda ulingoni, Novemba 28 kwenye ukumbi wa
Mlimani City Dar es Salaam kutetea ubingwa wa dunia wa Global Boxig
Council (GBC) kwa kupigana na bondia Hero Tito raia wa Indonesia.
Dk.
Mwakyembe aliyasema hayo jana katika sherehe ya Maltchoice ya kutimiza miaka 20
ya kutoa huduma ambayo ilifanyika Dar es Salaam.
“Katika kazi
zenu nimeona jinsi ambavyo mnasaidia kuendeleza michezo ikiwepo wasanii wa
filamu na riadha lakini naomba mnishike mkono katika pambano la Class
linatarajiwa kuchezwa hapa nchini baada ya mimi kusema litapigwa hapa
nyumbani,”
“Class ni
bondia kijana ana anafanya vizuri na sasa anatetea taji hilo ambalo alimpiga
bondia Jose Forero raia wa Panama Julai Mosi nchini Ujerumani uzani wa kati,”
aliongeza Dk. Mwakyembe.
Nje ya mkanda wa GBO pia Class anashikilia mikanda miwili ya ubingwa wa Afrika ya WBFP ambao
alimpiga bondia Mwansa Kabinga wa Zambia nchini kwao na UBO alimpiga Cosmas
Cheka
Class ambaye
alianza Ndondi Julai 2010 ameshapigana mapambano 24 na kushinda 20 huku 10
yakiwa kwa KO na amepigwa mapambano manne moja kwa KO.
Mpinzani
wake Tito alianza kupigana Februari 2004 ameshinda mapambano 23 kati yake nane
ni kwa KO amepigwa 12 na kwa KO 4 na ametoka sare mara mbili.
No comments:
Post a Comment