HATIMAYE
watatu wa kupanda Ligi Kuu ya England (EPL) wamekamilika baada ya Huddersfield
kuingia, huku wakiwa na mpango madhubuti wa kukabiliana na vigogo hapo, na wala
si kuingia tu kwa maana ya ushiriki.
Walifanikisha
kazi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa – Wembley, ambako ndio kwa kawaida huchezwa
mechi kubwa za kitaifa kama za kupata wanaoingia EPL, fainali za Kombe la FA,
Kombe la Ligi, pamoja na mechi za Timu ya Taifa ya England – Three Lions.
Hii ni mara
ya kwanza kwa Huddersfield wanaofundishwa na David Wagner kuingia ligi kuu,
ambapo maelfu ya washabiki wake waliingia mitaani Reading kwa ajili ya
kushangilia timu ilipopita kwenye basi kubwa la wazi.
Wanaungana
na Newcastle United wa Rafa Benitez na Brighton & Hove Albion kwenye
kimbembe cha EPL msimu ujao. Hii ni klabu ambayo shabiki wake mkubwa ni Waziri
Mkuu wa zamani, Harold Wilson.
Hali haikuwa
ya kawaida kwenye St George’s Square — lisilohusishwa kwa miaka mingi na
maandamano ya kupongeza timu kama hivi, lakini sasa kuna mwamko mpya na
burudani, kama ilivyokuwa Leicester, pale klabu hiyo walipotwaa ubingwa wa
England pasipo kutarajiwa.
Klabu tatu
hizi zinachukua nafasi zilizoachwa na Hull, Middlesbrough na Sunderland
walioshindwa kuhimili mnyukano kwenye ligi kubwa zaidi nchini England na
maarufu zaidi duniani iliyoshuhudia Chelsea wakitwaa ubingwa.
No comments:
Post a Comment