DEAL done! nyota wa Simba Ibrahim
Ajibu amemalizana na Yanga kwa kusaini mkataba wa miaka miwili na kwamba
ataitumikia klabu hiyo msimu ujao baada ya kutisha kwa misimu kadhaa
akiwa na wekundu hao wa mtaa wa Msimbazi.
Vuta nikuvute ya fundi huyo wa mpira na viongozi wake imechukua muda
mrefu lakini mwisho wa siku vigogo hao wakakubali kushindwa kimya kimya
ndipo viongozi wa Yanga walipotumia mwanya huo kumaliza biashara mapema
mchana wa leo.

Ibrahim Ajibu
Ajibu amepewa pesa
ya usajili Sh 50 milioni pamoja na gari ndogo ya kutembelea huku usajili
huo ukifanywa kwa siri kubwa ili kukwepa ‘msala’ walioupata baada ya
kumsajili beki wa kulia Hassan Ramadhan ‘Kessy’ akiwa hajamaliza mkataba
wake msimu uliopita.
Mkataba wa Ajibu na Simba utamalizika mapema mwezi ujao na viongozi
wa Yanga wamepanga kuweka hadharani kila kitu wakati huo huku sasa
wakipambana kukanusha kila kitu kuhusiana na uhamisho huo.
Huu unakuwa usajili wa pili kwa Yanga baada ya jana kumalizana na beki wa kati wa Taifa Jang’ombe Abdallah Hajji.
Post a Comment