ALIYEKUWA
kocha wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars', Charles Boniface Mkwasa
ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Yanga.
Mkwasa
ambaye aliwahi kuwa mchezaji na kocha wa Yanga anachukua nafasi iliyokuwa
inakaimiwa na Baraka Deusdedit anayerejea kwenye Idara ya Fedha.
Akizungumza
na wandishi wa habari jana Makao Makuu
ya klabu hiyo Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema Mkwasa anaanza
majukumu yake Februari mosi, mwaka huu.
"Mkwasa
ameteuliwa kushika wadhifa wa Katibu Mkuu nafasi ambayo ataanza kuitumikia
Februari mosi, tunampongeza na tunamtakia kila la heri kwenye majukumu haya
mapya," alisema Sanga
Akizungumza na gazeti hili, Mkwasa alishukuru uongozi wa Yanga kuona mchango wake na kumteuwa kwenye nafasi hiyo ya utawala.
Akizungumza na gazeti hili, Mkwasa alishukuru uongozi wa Yanga kuona mchango wake na kumteuwa kwenye nafasi hiyo ya utawala.
"Nashukuru
wameona mchango wangu kuanzia nikiwa mchezaji hadi kuwa kocha katika vipindi
tofauti, nawaahidi utumishi uliotukuka, zaidi anaomba ushirikiano,"
alisema Mkwasa.
Mkwasa
anarejea Yanga ikiwa ni mwezi mmoja umepita tangu aache kuwa kocha timu ya
taifa ya Tanzania, Taifa Stars, nafasi ambayo imechukuliwa na kocha Salum Mayanga.
Mkwasa aliifundisha Taifa Stars kuanzia Julai mwaka 2015 akirithi mikoba ya Mart Nooij na aliiongoza timu hiyo katika mechi 13, ikishinda mbili, kufungwa sita na sare tano.
Mkwasa aliifundisha Taifa Stars kuanzia Julai mwaka 2015 akirithi mikoba ya Mart Nooij na aliiongoza timu hiyo katika mechi 13, ikishinda mbili, kufungwa sita na sare tano.
No comments:
Post a Comment