SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), imesimamishwa Uwanja wa Jamhuri Morogoro kutumika ili kutoa
fursa kwa wamiliki kufanya marekebisho makubwa kwenye eneo la kuchezea.
Akizungumza na wandishi wa
habari jana, Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas alisema hatua hiyo imefikiwa
baada ya mchezo wa Mtibwa Sugar dhidi ya
Simba kuonekana sehemu ya kuchezea ikiwa kwenye hali mbaya hivyo inahitaji
marekebisho.
"Tumesimamisha matumizi ya
uwanja wa Jamhuri kupisha marekebisho endapo hayatafanyika, uwanja huo
hautatumika pia JKT Ruvu wameomba kuhama kutoka Mabatini kwenda Uwanja wa
Mkwakwani Tanga," alisema Lucas.
Pia uwanja wa Kichangani umeondolewa
kutumika kwa mechi za ligi, hivyo klabu za Iringa sasa timu zao zitatumia
Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini humo kwa mechi zao la ligi.
Lucas alisema baada ya mchezo
kumalizika mashabiki waliingia uwanjani kwa wingi na kusababisha usumbufu
mkubwa kwa wachezaji, waamuzi na waandishi wa habari hali ambayo ilisababisha kamera
ya Azam Tv kuangushwa na washabiki hao.
Pia Lucas alisema JKT Ruvu imeomba kubadilisha
uwanja wake wa nyumbani kutoka Mabatini Pwani kwenda Mkwakwani Tanga kutokana
na wachezaji wake 12 kwenda kwenye mafunzo ya kijeshi mkoani Tanga.
"Ombi hilo limekubaliwa kwa
mujibu wa Kanuni ya 6(6) ya Ligi Kuu, TFF/TPLB zina mamlaka ya mwisho kuhamisha
kituo cha mchezo kwa sababu inazoona zinafaa na kwa wakati husika,"
alisema Lucas.
TFF imewataka askari polisi kuwa
makini katika majukumu yao ya kusimamia usalama uwanjani na kuacha kutumia
nguvu kubwa katika kudhibiti fujo kwa wachezaji uwanjani.
No comments:
Post a Comment