Na Rahel
Pallangyo
SIMBA na
Azam FC zitashuka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza mchezo wao wa Ligi Kuu
baada ya serikali kufungulia uwanja huo ambao ulifungwa kutokana na mashabiki
wa Simba kung'oa viti wakati wa mchezo wa raundi ya kwanza dhidi yao na Yanga.
Katika
taarifa ya serikali ambayo ilitumwa kwenye vyombo vya habari na kusainiwa na
Kaimu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Zawadi Msalla inasema Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnaye ameridhishwa na ukarabati wa
miundo mbinu ya uwanja huo baada ya kuharibiwa Octoba Mosi, 2016.
"Nape
amewataarisha wapenzi wa michezo kutunza mali za serikali kwa manufaa ya
watanzania wote na kwa kushirikiana na vyombo vya usalama watawachukuliwa hatua
mtu mmoja mmoja kwani kamera zilizofungwa zitasaidia kuwabaini kila
atakayefanya tukio la uhalifu," alisema Zawadi.
Naye Afisa
Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, Alfred Lucas, alitoa shukrani kwa Waziri
Nape kwa niaba ya wadau na mashabiki wa soka Tanzania na kuwataka kuwa
wastarabu wanapokuwa ndani ya uwanja huo.
"Tunawaomba
watanzania na mashabiki wa soka kuwa na nidhamu na kushangilia kistaarabu kwani
uwanja mzima umefungwa kamera ambazo zina uwezo wa kuwatambua kila mmoja,"
alisema Lucas
Kwa upande
wa Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Simba, Haji Manara alisema kufunguliwa
kwa uwanja ni surprise kwao na kuwataka mashabiki wao kuwa na uvumilivu pindi
timu inapopata matokeo ambayo hayaridhishi.
"Tunawaomba
mashabiki wajitokeze kwa wingi kushangilia timu yao lakini pia wanatakiwa kuwa
na uvumilivu japo matokeo mengine yanasababishwa na maamuzi mabaya ya marefa
wetu, TFF mlifanyie kazi," alisema Haji.
Pia Haji
alisema timu ikifungwa kihalali hakuna mtu anayelalamika na kudai aliposema
mchezo dhidi ya mahasimu wao Yanga uchezeshwe na waamuzi toka nje ya nchi
alijua fika kanuni haziruhusu bali alifanya hivyo ili wabadilike.
Uwanja wa
Taifa ulifungwa na Waziri Nape kufuatia uharibifu uliofanyika Oktoba Mosi, 2016
kwenye mchezo wa Simba na Yanga mashabiki wa Simba wakipinga bao lililofungwa
na Amis Tambwe kwa madai kabla ya kufunga alikuwa ameshika mpira
Mchezo huo
uliochezeshwa na mwamuzi Martin Saanya ulimalizika kwa sare ya kufungana bao
1-1, bao la Simba likifungwa na Shiza Kichuya kwa mpira wa kona.
No comments:
Post a Comment