Waziri Nape ameyasema hayo mapema leo Jijini Dar es Salaam wakati wa kumpokea rasmi mwanariadha huyo tokea aliporejea kushiriki michuano mikubwa ya mbio za 14 za Standard Chartered Mumbai Marathon, nchini India na kuibuka shujaa zilizomalizika hivi karibuni.
“Serikali inajivunia kuwa na vijana wanailetea heshima Tanzania. Uzalendo wako Simbu ni chachu ya kwa vijana wengine kwani nao matamanio yao ni kushinda kama ulivyoshinda wewe tunakupongeza sana. Pia tunaipongeza Multichoice Tanzania kwa Uzalendo wa kuchukua jukumju la kumsimamia Simbu kwa muda wa mwaka mmoja, Tunataka na wadau wengine waige mfano kama huu wa Multichoice Tanzania kwani ni wa kizalenod” ameeleza Waziri Nape.
Na kuongeza kuwa, kuna mamlaka zingine zinatumia mabilioni ya pesa kupeleka kudhamini mambo mengine na kuacha vijana wenye kupeperusha bendera ya Tanzania nje ya Tanzania huku pesa hizo zikiteketea bure” amebainisha Waziri Nape.
Kwa upande wake, Simbu ameshukuru Serikali, wadau ikiwemo Multichoice, Wanahabari,familia yake na viongozi wa mchezo wa raidha hapa nchini kwa kumpa sapoti kwa kila anachokifanya kwani ameongeza juhudi na hali ambayo inamfanya aweze kufikia ushindi huo anaoupata kwa sasa.
Waziri wa Habari, utamaduni, michezo na Sanaa Mh. Nape Nnauye akisalimiana na mwanariadha Alphonce Simbu wakati wa tukio hilo.
Waziri wa Habari, utamaduni, michezo na Sanaa Mh. Nape Nnauye akiingia katika mkutano huo wa utambulisho
Waziri wa Habari, utamaduni, michezo na Sanaa Mh. Nape Nnauye akiwa na Mwanariadha Alphonce Simbu wakati wa tukio hilo
Mwanariadha Alphonce Simbu akielezea namna alivyoweza kuonesha maajabu yake na kuibuka
Waziri Nape akizungumza katika
tukio ambapo amewataka wadau kama Dstv kuendelea kujitokeza kusaidia
vipaji vya vijana hapa nchini
Waziri Nape akimvisha Mwanaraidha
Simbu medali yake aliyoshinda huko India, kuonyesha ishara ya kumpokea
na kutambua mchango wake
Meneja uendeshaji wa Multichoice
Tanzania, Ronald Shelukindo akipiga picha ya pamoja na Simbu pamoja na
zawadi zake alizoshinda nchini India.
Simbu akiwa na Medali yake
Simbu akionesha ushindi wake huo
Simbu akipiga picha ya pamoja na viongozi wa RT
No comments:
Post a Comment