MWANDISHI wa
Gazeti la HabariLeo na SpotiLeo, Rahel
Pallangyo amechaguliwa kuwa mjumbe wa kamati ya Utendaji wa Chama cha Waamuzi wa Soka Mkoa wa Dar es
Salaam kuwakilisha wanawake.
Rahel ambaye
pia ni kocha mwenye leseni B inayotambuliwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika
(CAF) alimwangusha mpinzani wake Isabela Kapera ambaye ni mwamuzi mstaafu wa
FIFA aliyepata kura moja dhidi ya tano za Rahel.
Nafasi ya
Mwenyekiti ilikwenda kwa Omar Abdulqudir aliyepata kura tano na Makamu
Mwenyekiti ni Sijali Mzeru aliyepata kura sita na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa
Taifa alichaguliwa Jovin Ndimbo kwa kura sita.
Katibu Mkuu
alichaguliwa Said Mbwana kwa kura tano, msaidizi ni Waziri Hunda aliyepata kura
sita na Mhazini ni Job Wandiba aliyepata kura sita.
Awali
akizungumza kwa niaba ya wenzake uongozi uliopita muda, Hemed Nteza alishukuru
kwa ushirikiano wa wajumbe na wachama kipindi chote walichokaa madarakani na
kuwaasa watakaochaguliwa kuendeleza umoja.
Naye
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Victor Mwandike alishukuru kwa kufanikisha
uchaguzi kufanyika na kushukuru wajumbe wa mkutano kamati yake kwa kushirikiana
vema.
"Nashukuru
wajumbe na mwanasheria wa kamati kwa kutusaidia kutafsiri vifungu vya katiba na
hatimaye tumemaliza kazi, nawatakia kila la heri katika kutekeleza majukumu
yenu," alisema Mwandike.
Katika hatua
nyingine Mwenyekiti mpya,
Abdulqudir aliwateua Hemed Nteza na Mzee
Malipula kuwa wajumbe wa heshima wa kamati ya utendaji.
No comments:
Post a Comment