Saturday, December 31, 2016
VITA YA WACHEZAJI LIGI YA ENGLAND LEO
ADAM LALLANA vs FERNANDINHO
Akianza kucheza ‘deeper role’ tofauti na zamani, Lallana amekuwa akifanya vema chini ya Klopp akiwa amefunga goli 11 na kufanya assist 12 na ana uwanja mkubwa katika kiungo kiasi cha kutengeneza uangalifu mkubwa kwa wapinzani.
Lallana hafanyi kazi ya ubunifu kama iliyokuwa akifanya majeruhi Philippe Coutinho lakini anafanya usaidizi mkubwa kwa washambuliaji na kutukimia fursa endapo anapata nafasi ya kufunga.
Fernandinho atakuwa na kazi kubwa ya kumzuia ingawa Jordan Henderson na Georginio Wijnaldum wana uwezo wa kusonga hadi eneo la kushambulia kwa pamoja.
ROBERTO FIRMINO vs NICOLAS OTAMENDI
Firmino hakuondolewa katika kikosi cha kwanza licha ya kuendesha gari akiwa amelewa katika mchezo dhidi ya Stoke, alifunga goli la pili na anaweza kupata nafasi katika kikosi cha kwanza katika mchezo dhidi ya City.
Klopp anapendezwa na tabia yake akiwa mazoezini na katika mechi, hupendelea kufungua nafasi na kumruhusu Sadio Mane kupita mbele yake kitu ambacho huvutia wakati wa mchezo.
Ki ukweli watakuwa wakimkaribia sana Otamendi, ambaye ana jukumu kubwa katika mchezo huu.
RAHEEM STERLING vs JAMES MILNER
Rahim Sterling amekuwa katika moto mkubwa kwa mara nyingine tena baada ya kupata kiwango chake wakati ambapo Milner akiwa vizuri katika kutengeneza mipira mingi kutoka kushoto.
Kuhusu Liverpool
Kiungo mchezeshaji wa Liverpool Philippe Coutinho hayuko fiti kuikabili Manchester City.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil amekuwa nje ya dimba kwa zaidi ya mwezi kutokana na kukabiliwa na maumivu ya kifundo cha mguu.
Pigo kubwa kuelekea mchezo huo dhidi ya kikosi chenye mbinu nyingi cha Pep Guardiola ambapo mlinzi wa kati Joel Matip, akiukosa mchezo huu ambao utakuwa ni mchezo wa nne kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu.
LIVERPOOL KIKOSI CHA AWALI:
Mignolet, Clyne, Lovren, Klavan, Milner, Henderson, Wijnaldum, Lallana, Mane, Origi, Firmino, Karius, Moreno, Alexander-Arnold, Lucas, Can, Ejaria, Sturridge, Woodburn.
Takwimu muhimu za mchezo
Mchezo wa mwisho na pekee kwa Manchester City kushinda dhidi ya Liverpool katika ligi ya Premier ndani ya dimba la Anfield (D5 L13) ulikuwa Mei 2003, magoli mawili ya Nicolas Anelka dhidi ya klabu yake ya zamani katika ushindi wa 2-1.
Sergio Aguero amefunga bao mara nne dhidi ya Liverpool katika ligi ya Premier lakini hakuna bao alilofunga akiwa Anfield.
Liverpool haijashindwa kufunga bao katika michezo 19 ya ligi ya Premier dhidi ya City.
Liverpool ilimaliza raundi ya kwanza kwa ushindi tangu 2014 (4-1 v Swansea City) na 2015 (1-0 v Sunderland).
Chelsea vs Stoke (Stamford Bridge)
Habari za vikosi
Chelsea
Pedro amesimama mchezo mmoja lakini Diego Costa na N’Golo Kante wanarejea tena katika kikosi cha kwanza wakati vinara wa msimamo wa ligi watakapokuwa wakikabiliana dhidi ya Stoke Jumamosi.
Mshambuliaji Costa na kiungo Kante wanatazamiwa kurudisha kasi na uzoefu wa kikosi baada ya kusimama mchezo mmoja kutokana na kufikisha kadi tano za njano katika mchezo dhidi ya Bournemouth Boxing Day.
Nahodha John Terry amerejea katika mazoezi kufuatia kupata majeraha ya mfupa wa ndani ya kalio lakini atasubiri kidogo kurejea katika uzima wake na kuingiza ushindani ndani ya kikosi.
CHELSEA KIKOSI CHA AWALI:
Courtois, Begovic, Ivanovic, Alonso, Fabregas, Zouma, Kante, Hazard, Loftus-Cheek, Moses, Costa, Matic, Willian, Batshuayi, Cahill, Terry, Azpilicueta, Chalobah, Luiz, Eduardo, Aina, Solanke.
Stoke City
Mlinzi Phil Bardsley anaweza kupata nafasi katika mchezo huu wa Jumamosi wakati wahunzi wa Stoke City watakapokuwa wanakabiliana na Chelsea katika dimba la Stamford Bridge.
Bardsley, aliumia mguu Novemba 19, lakini akianza mazoezi wiki hii.
Marko Arnautovic bado yuko kwenye adhabu, wakati ambapo Marc Muniesa, Geoff Cameron (wote wana maumivu ya mguu) na Jack Butland (kifundo) wote watakosekna.
STOKE CITY KIKOSI CHA AWALI
Grant, Given, Shawcross, Martins Indi, Johnson, Pieters, Bardsley, Whelan, Imbula, Adam, Allen, Bojan, Afellay, Shaqiri, Sobhi, Diouf, Walters, Crouch, Bony.
Takwimu muhimu za mchezo
Chelsea ilishindwa kuifunga Stoke City msimu uliopita (D1 L1), hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Chelsea kushindwa kuifunga Stoke katika michezo yote ya uwanja wa nyumbani na ugenini tangu 1974/75.
Wahunzi hawajashinda katika michezo 11 kila wanapoifuata Chelsea, ushindi wao wa mwisho ulikuwa ni 1-0 mwezi April 1974.
Stoke imeshinda michezo mitatu kati ya michezo 8 iliyocheza Stamford Bridge.
Leicester vs West Ham (Saturday, King Power Stadium)
Habari za vikosi
Leicester
Robert Huth na Christian Fuchs watakuwepo katika kikosi cha Leicester kuikabili West Ham baada ya kumaliza adhabu ya kusimama mchezo mmoja kutokana na kufikisha kadi 5 za njano.
Jamie Vardy atakosekana baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu alipata wakati wa mchezo dhidi ya Stoke na ataukosa mchezo huu na mwingine dhidi ya Middlesbrough.
Riyad Mahrez atakuwa akirejea kuwekwa benchi na meneja Claudio Ranieri katika mchezo wa Boxing Day ambao Leicester ilipoteza 2-0 mbele ya Everton ilhali Andy King atakuwa akifikisha mchezo 350 katika kikosi cha Leicester.
LEICESTER KIKOSI CHA AWALI:
Schmeichel, Zieler, Hamer, Simpson, Fuchs, Morgan, Huth, Hernandez, Wasilewski, Chilwell, Schlupp, Drinkwater, James, King, Mendy, Amartey, Mahrez, Albrighton, Musa, Gray, Ulloa, Okazaki, Slimani.
West Ham
West Ham itakuwa ikimtumia kiungo Pedro Obiang katika mchezo huu dhidi ya Leicester.
Kiungo huyo alikosekana katika nchezo wa Boxing Day dhidi ya Swansea kutokana na kufikisha kadi 5 za njano.
WEST HAM KIKOSI CHA AWALI:
Randolph, Adrian, Collins, Ogbonna, Reid, Kouyate, Masuaku, Antonio, Cresswell, Noble, Obiang, Fernandes, Nordtveit, Payet, Feghouli, Ayew, Carroll, Fletcher.
Takwimu muhimu
Leicester haijafungwa michezo mitatu ya mwisho ya ligi ya Premier dhidi ya West Ham (W2 D1) lakini hawajacheza michezo 4 bila kupoteza dhidi ya washika nyundo.
Mchezo wa mwisho West Ham kushindwa kufunga goli dhidi ya Leicester ulikuwa ni Agosti 2004 ( kwenye Championship).
Watford vs Tottenham (Sunday, Vicarage Road)
Habari za vikosi
Watford
Watford huenda ikawakosa wachezaji wake muhimu 9 katika mchezo huu wa mkesha wa mwaka mpya.
Walter Mazzarri leo alikuwa akitangaza wachezaji ambao huenda akawakosa kuelekea mchezo huu katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Ben Watson anamatatizo ya familia, wakati ambapo Adrian Mariappa na Roberto Pereyra (wana maumivu ya mguu), Daryl Janmaat, Valon Behrami na Isaac Success (wote maumivu ya msuli) kama ilivyo kwa Stefano Okaka (msuli) na Craig Cathcart (hayuko fiti) pia Miguel Britos ana kadi 5.
WATFORD KIKOSI CHA AWALI:
Gomes, Zuniga, Cathcart, Prodl, Holebas, Capoue, Kaboul, Guedioura, Deeney, Amrabat, Okaka, Pantilimon, Mason, Kabasele, Ighalo, Sinclair.
Tottenham
Toby Alderweireld atakuwa anarejea baada ya kuugua na hivyo atakuwa akiimarisha ulinzi katika mchezo huu dhidi ya Watford.
Jan Vertonghen na Kyle Walker wote wataukosa mchezo huu kufuatia kukamilisha kadi 5 za njano.
TOTTENHAM KIKOSI CHA AWALI
Lloris, Vorm, Lopez, Rose, Davies, Alderweireld, Dier, Carter-Vickers, Wimmer, Trippier, Wanyama, Winks, Dembele, Eriksen, Alli, Sissoko, Onomah, Nkoudou, Son, Kane, Janssen.
Takwimu muhimu
Watford haijawa na matokeo mazuri dhidi ya Tottenham katika ligi ya Premier mbali ya kwenda sare mara mbili na kufungwa mara 4.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment