MCHEZAJI
Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara anatarajiwa kujulikana leo wakati wa utoaji tuzo
mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Taarifa
iliyotolewa na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas
jana ilisema aina 13 ya tuzo zitatolewa leo.
Alisema
wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora ambaye mshindi atazawadiwa Sh 9,228,820 na timu zao katika mabano ni Shiza Kichuya
(Mtibwa Sugar), Juma Abdul (Yanga) na
Mohamed Hussein (Simba).
Tuzo ya Kipa
Bora ambayo zawadi yake ni Sh 5,742,940, inawaniwa na Aishi Manula (Azam), Beno
Kakolanya (Tanzania Prisons) na Deogratius Munishi (Yanga).
Mchezaji
Bora wa Kigeni ambaye atazawadiwa fedha taslimu kama ya kipa bora ni Donald Ngoma (Yanga), Thabani Kamusoko
(Yanga) na Vincent Agban (Simba), huku Kocha Bora akizawadiwa Sh milioni nane,
ambapo wanaowania ni Hans Van Pluijm
(Yanga), Mecky Maxime (Mtibwa Sugar) na
Salum Mayanga (Tanzania Prisons).
Wanaowania
tuzo ya Mwamuzi Bora ni Anthony Kayombo, Ngole Mwangole na Rajab Mrope, ambao
mshindi atapata kiasi cha Sh milioni 5.7, huku Mchezaji Bora Chipukizi
akizawadiwa Sh milioni nne, ambapo wanaowania ni Farid Mussa (Azam), Mohamed Hussein (Simba), Mzamiru Yasin
(Mtibwa Sugar) na Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar).
Pia kutakuwa
na zawadi ya Goli Bora la Msimu, wanaowania ni Ibrahim Ajib wa Simba na Amis
Tambwe wa Yanga na mshindi atapata Sh milioni tatu.
Zawadi
nyingine ni ya timu bingwa itakayopata Sh milioni 81, makamu bingwa Sh milioni
40, mshindi wa tatu sh milioni 29 na mshindi wa nne Sh milioni 23, huku timu
yenye nidhamu ikipata Sh milioni 17.
Yanga ndiyo
bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam imeshika nafasi ya pili, Simba ya tatu
na Prisons ya nne.
Cio…
No comments:
Post a Comment