Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, July 28, 2016

TAMASHA KUBWA LA DANSI KUFANYIKA KESHO LEADERS CLUB.






Na Rahel Pallangyo
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda,  ameahidi kutoa zawadi ya milioni moja kwa bendi itakayofanya vizuri kwenye Tamasha la bendi mbalimbali za muziki wa dansi zinatarajia  litakalofanyika  leo kwenye viwanja vya Leader Club Kinondoni. 
Ahadi hii Makonda aliitoa mbele ya wanamuziki hao wa dansi ambao walikwenda ofisini kwake kumtaarifu adhima ya tamasha hilo ambalo sehemu ya mapato itatumika kuchangia madawati.
"Najua nyimbo za dansi zinatoa ujumbe mzuri wenye kuelimisha tofauti na hizi za muziki wa kizazi kipya ambao mara nyingi wanaimba mapenzi naahidi bendi itakayotoa burudani nzuri nitaipa zawadi ya milioni moja", alisema Makonda na kushangiliwa na wanamuziki hao.
Pia Makonda alisema anatarajia kuwapo pia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, atakuwepo kupata burudani kwani si kila muda mafaili tu.
Naye Ally Choki akizungumza kwa niaba ya wenzake alisema wanatarajia kutoa burudani kali kwa mashabiki kwani muziki utapigwa live.
"Tamasha hili ni la kwanza Tanzania na linatoa fursa kwa wanamuziki wa dansi wakongwe na chipukizi kukutana kwenye jukwaa moja hali ambayo itajenga umoja na kikubwa kuchangia madawati ili kuboresha elimu kwa wadogo na watoto wetu "Alisema Choki.
Bendi zitakazotumbuiza kwenye tamasha hilo ambalo limeandaliwa na kampuni ya Tanzania band Festival ni Msondo Ngoma, Mlimani Park Orchestra,The African stars band, Fm Academia band, Mapacha watatu, Ya moto bend, B band ya Banana Zorro, Top band ya TID, Skylight bend,  La capitale ya King Kii na bendi nyingine nyingi.
Kiingilio ni 15000 na tamasha litaanza saa tano asubuhi na kumalizika usiku wa manane

No comments:

Post a Comment