Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, July 28, 2016

MAN CITY MBIONI KUMNASA STONE WA EVERTON

Manchester City wanaongea na Everton ili mununua John Stones ingawa dili bado ipo mbali kukamilika.
Inaaminika City itapaswa kulipa Pauni Milioni 50 kumnunua Mchezaji huyo wa zamani wa Timu ndogo Barnsley ambae Mwaka Jana nusura ajiunge na Chelsea.
Stones, ambae alikuwemo Kikosi cha England kilichocheza EURO 2016 Mwezi Juni bila yeye kucheza hata Mechi moja, alianza kuichezea Barnsley Machi 2012 na Miezi 10 baadae kuhamia Everton.
Bosi wa City, Pep Guardiola, amevutiwa sana na Sentahafu huyo hasa kwa vile anafiti staili yake ya uchezaji na amefafanua.

“Kawaida Masentahafu huwa na nguvu na wazuri hewani. Lakini tunahitaji kujenga mashambulizi toka nyuma na kufanya Kiungo wafunguke na kutoa pasi rahisi kwa Mastraika!”

Huko nyuma, Guardiola ashawahi kuwatumia Viungo kama Masentahafu wakati yuko Barcelona na Bayern Munich kwa kuwachezesha Viungo Javier Mascherano na Javi Martinez nafasi hizo.
Huko City tayari ashamgundua Kiungo wa Brazil, Fernandinho, kuwa anafaa kazi ya kuwa Beki.

Guardiola ameeleza: “Fernandinho anaweza kucheza nafasi 10 tofauti. Ni mwepesi, ana haraka sana, ana akili, mpiganaji. Ana nguvu hewani na ana kipaji cha kujenga mashambulizi, anaweza kwenda kulia au kushoto na kutoa pasi ndefu!”

No comments:

Post a Comment