WAPINZANI wa Yanga, timu ya TP Mazembe inatarajiwa
kuwasili kesho na msafara wa watu 32 kwa ajili ya mchezo wa kombe la Shirikisho
barani Afrika utakaochezwa Jumanne Uwanja wa Taifa.
Akizungumza na wandishi wa habari leo, Afisa Habari
wa Shirikiso la Soka Tanzania, Alfred Lucas alisema, TP Mazembe wametuma
taarifa kuwa watawasili leo na mahali watakapofikia ila muda gani watafika
hawajasema.
“TP Mazembe wametuma taarifa kuwa watawasili kesho lakini hawajasema watashuka saa ngapi lakini tunaendelea kuwasiliana nao
ili tuweze kuandaa watu wa usalama watakaowapokea kwa sababu TFF ndio
wanaratibu kila kitu kwaniaba ya CAF”, alisema Lucas.
TP Mazembe ambao inaongoza kundi A wakiwa na pointi
tatu wanakuja kucheza na Yanga ambao hawana pointi baada ya kupoteza mchezo
uliopita dhidi ya Mo Bejaia.
Yanga wamerejea jana wakitokea Uturuki baada ya mchezo
huo ambapo ilikuwa imeweka kambi awali kwa ajili ya maandalizi ya kuikabili TP
Mazembe, mabingwa wa Afrika msimu uliopita.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa
ukichagizwa na mashabiki wa Simba ambao wanatarajiwa kuishangilia TP Mazembe
kulipiza kisasi kwa Yanga baada kuishangilia walipokuja kucheza na Simba miaka
mitano iliyopita.
No comments:
Post a Comment