Timu ya Taifa ya
vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) Imeingia kambini leo kujiandaa na
mchezo wa kufuzu fainali za kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya vijana
wenzao wa Shelisheli utakaofanyika Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa,
jijini Dar es Salaam.
Katika kuajindaa na
mchezo huo, Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano
ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth
Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika
Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
Kadhalika Serengeti
Boys ilicheza mfululizo michezo saba ya kimataifa bila kufungwa dhidi ya Misri
(2), India, Korea Kusini, Malaysia na Marekani (USA). Kabla ya hapo timu hiyo
ilicheza michezo kadhaa ya ndani na timu za chini ya umri wa miaka 20 bila
kupoteza hata mchezo mmoja.
Katika mashindano ya
AIFF, timu hiyo pekee kutoka Afrika na ambayo ilikua kipenzi cha mashabiki
katika jiji la Goha ilicheza na timu ambazo ziko juu katika hatua za juu katika
mtoano wa kuwania kushiriki Kombe la Dunia kupitia mabara yao yaani CONCACAF
(USA) na AFC (India, Korea na Malaysia).
Mchezo wa marudiano
kati ya Serengeti Boys na Shelisheli utachezwa Julai 2, 2016 huko Shelisheli.
No comments:
Post a Comment