Rais wa zamani wa
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Sepp Blatter amefunguka kuhusu upangaji wa
mashindano ya Ulaya na kueleza kuwa kuna mchezo ambao umekuwa ukifanyika wakati
wa upangaji wa michezo hiyo.
Akifanya mahojiano na
kituo cha La Nacion, Blatter ameeleza kumekuwepo na upangaji wa michezo kwa
kutumia mipira ambayo inakuwa ndani ya kapu la kuchanganyia mipira na
wanachokifanya ni anayekwenda kuchagua mpira anatumia mpira ambao unakuwa na
joto au unakuwa na kawaida.
“Ndiyo, nimeona kwa
macho yangu ni kama usaliti … ni katika mashindano ya Ulaya. Unaweza kuona
inatumika mipira kwa kuwa ya moto au ya baridi. Nina ushahidi wa hilo.
“Sijawahi kuchota
sana mipira, marais wengine walifanya zaidi kwa kuchukua wao wenyewe mipira
kutoka katika kikapu,” alisema Blatter.
No comments:
Post a Comment