Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Jamal Malinzi amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha John
Mabula - mchezaji wa zamani wa timu ya soka ya Mtibwa Sugar ya Morogoro inayoshiriki
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Mbali ya Mtibwa Sugar, taarifa za Mabula ambaye pia
amewahi kuchezea Moro United ya Morogoro na Shinyanga Shooting ya Shinyanya kwa
mafanikio nafasi ya ulinzi kwa muda mrefu katika timu hizo, aliuawa kwa
kuchomwa kisu na mwenzake alipokuwa akiamulia ugomvi huko Kitunda - nje kidogo
ya Jiji la Dar es Salaam.
Rais Jamal Malinzi amemwelezea Mabula kuwa ni
mchezaji aliyekuwa na uwezo na uadilifu na mchango wake katika soka utabaki
katika dhana ya kumbukumbu ya wachezaji mahiri wa Tanzania waliotokea kucheza
nafasi ya ulinzi japokuwa ametangulia mbele za haki.
Rais Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa
uongozi wa timu ambazo alicheza ambazo ni Mtibwa Sugar, Moro United na
Shinyanga Shooting; kadhalika familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki
walioguswa na msiba huo wa gwiji huyo aliyepata pia kucheza timu ya taifa ya Vijana
wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ ya mwaka 2002-2004.
Rais Malinzi amewaasa wadau wote kuwa watulivu
wakati huu mgumu wa msiba wa mpendwa wetu Mabula hasa kutokana na mazingira ya
kifo. Bwana alitoa, Bwana Ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe. Amina.
No comments:
Post a Comment