Manchester United imetangaza rasmi kuwa Kiungo wao Mkongwe Michael Carrick amesaini Mkataba wa kumbakisha kwa Mwaka mmoja zaidi hadi Juni 2017. Carrick,
mwenye Miaka 34, alisaini kuichezea Man United kwa mara ya kwanza Julai
2006 na tangu wakati huo amemudu kuisaidia Klabu kutwaa Ubingwa wa Ligi
Kuu England mara 5, FA CUP, Kombe la Ligi, Kombe la Klabu Bingwa na
Ubingwa wa UEFA CHAMPIONS LIGI. Akiongea
mara baada ya kusaini Mkataba mpya baada ya ule wa awali kumalizika,
Carrick alisema: “Hii Klabu kubwa kabisa imekuwa sehemu ya maisha yangu
kwa Miaka 10, na hivyo nina furaha sana hii safari ya ajabu inaendelea.
Ni jambo kubwa sana kupata fursa hii kufanya kazi chini ya Jose Mourinho
ambae ana mafanikio makubwa. Napenda kuwashukuru Mashabiki kwa sapoti
yao isiyoyumba. Kutwaa FA CUP ilikuwa ni wakati spesho na, tunatarajia,
tutatwaa Mataji mengi baadae.” Nae
Meneja mpya wa Man United, Jose Mourinho, alizungumza kuhusu Carrick
kubaki: “Michael ni Kiungo mwenye akili sana na msomaji mzuri wa gemu.
Nimefurahi sana ameongeza Mkataba. Fomu yake Mwaka huu inaonyesha uwezo
wake na furaha yake mchezoni bado iko juu kabisa. Michael ana utajiri
mkubwa wa uzoefu kwa kukaa kwake Klabuni hapa Miaka mingi na uzoefu wake
utanisaidia sana. Ninangoja kwa hamu kubwa kufanya nae kazi.” Hiii
ni habari nyingine njema kwa Mashabiki wa Man United ambao Jana
walipokea kwa shangwe pale ilipoyangazwa kuwa Mourinho amesaini Mchezaji
wake wa kwanza baada kumsaini Eric Bertrand Bailly ambae aliekamilisha
Uhamisho wake kutoka Villarreal CF ya Spain.
EYONG AFUNGA BAO PEKEE CAMEROON YAICHAPA GABON 1-0
-
BAO la dakika ya sita la mshambuliaji wa Levante ya Hispania, Karl Edouard
Blaise Etta Eyong limeipa Cameroon ushindi wa 1–0 dhidi ya Gabon katika
mchezo...
Stronger Together. Ready for 2026.
-
*@Pictures by Mobila Safaris Team-Serengeti.*
*Stronger Together. Ready for 2026.*
Dear Partner,
As 2025 draws to a close, we want to thank you for...
Post a Comment