Friday, June 3, 2016
JUMA ABDUL NA SHIZA KICHUYA WAKABIDHIWA TUNZO ZAO NA VODACOM
Beki wa Yanga, Juma Abdul na kiungo wa Mtibwa Sugar, Shiza Kichuya wamekabidhiwa hundi zao baada ya kila mmoja kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara wa mwezi.
Wachezaji hao wamekabidhiwa hundi zao na Afisa Matukio na Udhamini wa kampuni ya Vodacom, Ibrahim Kaude, ambayo ndio wadhamni wakuu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara huku Afisa wa bodi ya ligi, Joel Balisidya akishuhudia
Juma ambaye aliibuka mchezaji bora wa mwezi Aprili na Kichuya ambaye alikuwa mchezaji bora wa mwezi Machi waliishukuru Vodacom kwa kuwakadhini zawadi zao.
“Tunaishukuru Vodacom kwa kutupatia zawadi zetu na tunaahidi kuwa mabalozi wazuri na tutaongeza juhudi kuanzia kwenye timu yangu hadi kwenye timu ya Taifa”, alisema Juma.
Juma aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Aprili, 2016 baada ya kura zake kuwashinda Donald Ngoma ambaye pia anacheza Yanga na Hassan Dilunga wa JKT Ruvu ya Pwani
Wachezaji bora wa miezi mitatu iliyopita kabla ya Abdul na Kichuya ni kiungo Thaban Kamusoko wa Yanga (Desemba 2015), beki Shomari Kapombe wa Azam (Januari 2016), Mshambuliaji Mohamed Mkopi wa Tanzania Prisons (Februari 2016)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment