MWENYEKITI wa klabu ya
Yanga, Yusuph Manji amechukua fomu ya kuendelea kutetea nafasi hiyo
katika Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Juni 11.
Manji ambaye anakubalika
kwa wanachama wa klabu hiyo aliambatana na makamu Mwenyekiti wa klabu
hiyo Clement Sanga katika zoezi la uchukuaji wa fomu huku mamia ya
wapenzi wa Yanga wakilipuka kwa furaha.
Manji amewambia
waandishi wa Habari pamoja na wanachama wa timu hiyo waliohudhuria
katika makao makao makuu ya klabu kuwa anataka kuendelea kuongoza kwa
ajili ya maendeleo ya Yanga.
"Nachukua fomu hii
nikiwa na machungu na maendeleo ya klabu hii na nia yangu ni kupata
mafanikio zaidi ya hapa tulipofika," alisema Manji.
Katika hatua nyingine
Manji amemsimamisha uanachama Mwenyekiti wa matawi ya klabu hiyo, Mzee
Mohammed Msumi baada ya kugundulika kutaka kuhujumu mchakato wa uchaguzi
kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa TFF na BMT.
Manji alitoa ushahidi wa
sauti iliyosikika Mwenyekiti huyo akipanga mikakati ya kukatwa jina la
Manji katika Uchaguzi ili kumrejesha katibu mkuu wa zamani, Jonas
Tiboroha.
"Kwa mamlaka niliyonayo
kama Mwenyekiti nimemsimamisha uanachama Msumi kwa kupanga hujuma dhidi
yangu katika Uchaguzi huu," alisema Manji.
No comments:
Post a Comment