LEJENDARI
wa Soka Duniani anaetoka Brazil Pele amemshauri Kinda wa Manchester
United Marcus Rashford kutoonyesha woga wakati Mchezaji huyo alieibuka
Msimu huu akijitayarisha kuichezea England kwenye Fainali za Mataifa ya
Nchi za Ulaya EURO 2016 zitakazoanza huko France Juni 10.
Rashford, mwenye Miaka 18, alishangaza
ulimwengu pake alipocheza Mechi yake ya kwanza tu na Man United dhidi ya
FC Midtylland kwenye EUROPA LIGI na kupiga Bao 2 na Siku 3 baadae
kupiga tena Bao 2 wakati Man United inaitwanga Arsenal kwenye Ligi Kuu
England. Tangu wakati huo, Rashford ameichezea Man United Mechi 18 na kupiga Bao 8. Kocha
wa England Roy Hodgson akaamua kumchukua Kinda huyo Kikosini mwake na
katika Mechi ya Kwanza tu kuichezea England Ijumaa iliyopita Rashford
alifunga Bao la Kwanza wakati England inaichapa Australia 2-1 na kuvunja
Rekodi ya tangu 1938 ya kuwa Kijana mdogo kabisa kufunga Bao katika
Mechi yake ya kwanza ya England. Sasa Lejendari Pele, anaesifika
kuwa ndie Mchezaji Bora kabisa katika Historia ya Soka na ambae ndie
Mchezaji pekee alietwaa Kombe la Dunia mara 3, la kwanza akiwa na Miaka
17 tu, amempa ushauri Rashford. Pele
amesema: "Leo umri si muhimu. Muhimu kuwa tayari . Lakini daima, daima
usiwe na woga. Namtakia bahati ile ile niliyopata katika maisha yangu ya
Soka. Kuna presha kubwa lakini anapaswa kujiamini." Pele ameeleza:
"Kabla sijatwaa Kombe la Dunia kwa maracya kwanza, Makocha walinieleza -
upo hapa kwa sababu una staili, ni Mchezaji mzuri, usiogope kwa sababu
Wachezaji wengine ni wakubwa kupita wewe. Huu ni ujumbe wangu kwa
Rashford!" Kwenye EURO 2016 England wapo Kundi B na wataanza Juni 11 kucheza na Russia kisha Wales na Slovakia.
Wamachinga Dar wakemea uvunjifu wa amani
-
wadai suluhu ya changamoto haitatuliwi kwa uvunjifu wa amani.
Na Mwandishi Wetu
Umoja wa wa Wajasiriamali wa Mkoa wa Dar es Salaam umewataka Watanzania...
Stronger Together. Ready for 2026.
-
*@Pictures by Mobila Safaris Team-Serengeti.*
*Stronger Together. Ready for 2026.*
Dear Partner,
As 2025 draws to a close, we want to thank you for...
Post a Comment