KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(TASWA) ilikutana Dar es Salaam Mei 24, 2016 kujadili masuala mbalimbali.
A; Tuzo za
Wanamichezo Bora
Kikao kilikubaliana Tuzo za Wanamichezo Bora zinazotolewa kila mwaka na
TASWA, safari hii zifanyike Agosti 26, mwaka huu, Dar es Salaam zikihusisha
michezo mbalimbali.
TASWA imeuanda kamati maalum kwa ajili ya kusimamia upatikanaji wa
wanamichezo hao bora, kamati ambayo inajumuisha waandishi waandamizi kutoka
vyombo mbalimbali vya habari na wataalamu kutoka vyama mbalimbali vya michezo.
Sekretarieti ya TASWA inaendelea kufanya mawasiliano na wateule wa kamati hiyo
kabla ya kuwatangaza.
Kwa kawaida kila mwaka TASWA inatoa tuzo kwa wanamichezo bora wa kila
mchezo na pia kunakuwa na mwanamichezo bora wa jumla kwa mwaka husika.
Baadhi
ya waliopata kutwaa tuzo ya Mwanamichezo Bora Tanzania wa jumla kwa miaka kumi
iliyopia na miaka yao katika mabano ni Samson Ramadhani (2006), Martin Sulle
(2007) na Mary Naali (2008) wote wanariadha.
Mwaka
2009 tuzo ilienda kwa mcheza netiboli Mwanaidi Hassan, ambaye pia alitwaa tuzo
hiyo mwaka 2010, wakati mwaka 2011, ambapo tuzo yake ilitolewa mwaka 2012
mshindi alikuwa mwanasoka Shomari Kapombe. Mwaka 2013/2014 ilienda kwa
mwanasoka Sheridah Boniface.
Mwaka
2015 tuzo ilifanyika katika aina nyingine,
ambapo walizawadiwa wanamichezo 10 tu waliofanya vizuri zaidi katika
miaka 10 ya urais wa Jakaya Kikwete na pia TASWA ilitoa Tuzo ya Heshima kwa
Kikwete.
B; Media Day
Kama inavyojulikana
chama chetu kimekuwa kikiandaa bonanza maalum likihusisha waandishi na
wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini, lakini kwa miaka
miwili bonanza hilo limekwama kufanyika kutokana na sababu mbalimbali. Kikao
kimekubaliana nguvu zaidi ielekezwe ili jambo hilo lifanyike na kuwapa raha
wadau. Taarifa zaidi kuhusu Media Day itatolewa Jumamosi wiki hii.
C: Changamoto kwa
waandishi
Kikao
kilijadili changamoto mbalimbali zinazowakabili waandishi wa habari za michezo
na chama kwa ujumla, ambazo zimewekewa mikakati ya muda mfupi na mrefu na
utekelezaji wake utaanza kuonekana siku chache zijazo.
Ahsanteni,
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
25/05/2016
No comments:
Post a Comment