Shirikisho la vyama vya soka Afrika
CAF limepanga kuipanua michuano yake ya ngazi za Klabu, ile ya Klabu bingwa na
ile ya Shirikisho katika hatua ya makundi kutoka timu nane za sasa mpaka kumi
na sita ifikapo mwaka 2017. Hayo yamesemwa jana Jumatano huko Mexico na Rais wa
shirikisho hilo Issa Hayatou wakati akiongea na wakuu wa soka toka Afrika
wanaohudhuria mkutano wa FIFA unaoendelea nchini humo. Hayatou amesema muundo
huo mpya utashirikisha makundi manne madogo madogo ya timu nne nne badala ya
muundo wa sasa ambao umekuwa ukishirikisha makundi mawili ya timu nne nne
ambapo washindi wa kwanza na wa pili wa kila kundi hufuzu hatua ya nusu finali.
Wakati huohuo Hayatou amesema kuwa muundo huo mpya utaenda sambamba na
uboreshwaji wa zawadi za fedha kwa washindi wa michuano hiyo hii ni baada ya
CAF kuingia mkabata mpya wa miaka 12 wa matangazo na masoko [Media and
Marketing] wenye thamani ya zaidi ya dola Bilioni moja. Kwa sasa mshindi wa
Ligi ya mabingwa hupata kitita cha dola milioni $1.5 na bingwa wa Shirikisho
hupata dola $660,000.
No comments:
Post a Comment