KOCHA Mkuu wa Azam FC, Zeben Hernandez amesema amefurahi
kuja Tanzania kwani anaamini kuna vipaji kama Farid Mussa anayecheza soka
Hispania.
Zeben Hernandez ambaye atakuwa kocha Mkuu endapo
watakubalia na uongozi wa Azam FC, atakuwa akisaidiwa na Jonas Garcia walipokelewa leo na Saad Kawemba Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
(JNIA)
Makocha hao ambao
raia wa Hispania wametoka klabu ya Deportivo Tenerife ya nchini humo.
Akizungumza na gazeti hili wakala wa makocha hao Rayco
Garcia alisema kuwa makocha hao wamevutiwa kuja Tanzania baada ya kuona kiwango
cha mshambuliaji Farid Musa ambaye amesajiliwa na klabu hiyo ya daraja la
kwanza akitokea Azam FC.
“Makocha hawa wamekuja Tanzania baada ya kuridhishwa na
kiwango cha mchezaji Farid na wanaamini kuna vipaji vingi,” alisema Rayco
Makocha hao watasafiri
kwenda Tanga leo kuiona Azam FC, ikicheza na African Sports katika mchezo wa
Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Tayari kocha Muingereza, Stewart John Hall amekwishaaga kwamba ataondoka mwishoni mwa msimu, ambao unakamilika Juni.
Tayari kocha Muingereza, Stewart John Hall amekwishaaga kwamba ataondoka mwishoni mwa msimu, ambao unakamilika Juni.
No comments:
Post a Comment