DANNY
WELBECK atakuwa nje ya Uwanja kwa Miezi 9 baada kufanyiwa upasuaji
kwenye Goti lake la Kulia kwa mujibu wa ripoti toka Klabuni Arsenal.
Welbeck aliumia Jumapili huko Etihad wakati Arsenal ikitoka Sare 2-2 na Manchester City kwenye Mechi ya Ligi Kuu England. Taarifa ya Arsenal imesema Welbeck ameumia vibaya Goti lake la Kulia na kulazimika kufanyiwa operesheni na ili apone kabisa anahitaji Miezi 9 ya kujiuguza na hilo litamfanya akose kuichezea England kwenye Fainali za Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, itakayochezwa Nchini France kuanzia Juni 10.
Hili ni pigo kubwa kwa Arsenal na Welbeck, mwenye Miaka 25, ambae alirejea tena Uwanjani katikati ya Februari baada ya kuwa nje ya Uwanja kwa Miezi 9 na Nusu akiuguza Goti lake jingine.
Tangu arejee Uwanjani, Welbeck aliichezea Arsenal Mechi 15 na kufunga Bao 5 na katika Mechi yake ya kwanza aliporejea tu ndie alifunga Bao la ushindi dhidi ya Mabingwa wapya Leicester City.
Hata kwa Meneja wa England, Roy Hodgson, kukosekana kwa Welbeck ni pigo kwani kwenye Mechi za kuwania kutinga Fainali za Makundi za EURO 2016 Welbeck alifunga Bao 6 akipitwa tu na Kepteni Wayne Rooney aliepiga Bao 7.
No comments:
Post a Comment