Kikosi cha
timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro
Premium Lager, kinatarajiwa kuwasili leo saa 8 usiku katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Mwl. JK Nyerere kikitokea nchini Chad kilipokuwa na mchezo dhidi
ya wenyeji jana jioni.
Msafara wa
Taifa Stars unaongozwa na mkuu wa msafara ambaye pia ni Rais wa Chama cha Soka
Zanzibar (ZFA), Ravia Idarus Faina utaondoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa
N’Djamena saa 8 mchana kuelekea Addis Ababa nchini Ethiopia, kabla ya
kuunganisha ndege saa 4 usiku tayari kwa safari ya kurejea nyumbani Tanzania.
Stars
inarejea nyumbani baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya wenyeji Chad,
bao lililofungwa na nahodha Mbwana Samatta katika mchezo uliochezwa uwanja wa
Omnisport Idriss Mahaymat Ouya jijini N’Djamena katika mchezo wa kundi G
kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2017.
Mara baada
ya kuwasili jijini Dar es salaam, kikosi cha Taifa Stars kitaingia moja kwa kwa
moja kambini katika hoteli ya Urban Rose iliyopo eneo la Kisutu kujiandaa na
mchezo wa marudano utakaochezwa siku ya Jumatatu ya Pasaka katika uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment