MENEJA
mpya wa Man City Pep Guardiola atapambana na Mahasimu wao wakubwa
Manchester United katika Mechi zake za kwanza Klabuni hapo katika
wadhifa wake mpya.
Klabu hizi za Manchester zitakutana huko Bird's Nest Stadium huko Beijing, China, Jumatatu Julai 25 ikiwa ni moja ya Mechi za Kirafiki kwa ajili ya kujitayarisha na Msimu mpya ambapo Timu kubwa Duniani hujumuishwa kwenye Mashindano ya kugombea International Champions Cup. Mwishoni mwa Msimu huu, Guardiola atambadili Bosi wa sasa City Manuel Pellegrini.
Kwenye Mashindano ya safari hii ya International Champions Cup, Leicester City, ambao wameshangaza wengi kwa kuongoza Ligi Kuu England kwa muda mrefu, pia wamepangwa kucheza na Barcelona na Paris St-Germain.
Msimu mpya wa Ligi Kuu England wa 2016/17 utaanza Agosti 13.
FA CUP:
Mechi ya Marudiano ya Robo Fainali ya EMIRATES FA CUP kati ya West Ham na Manchester United itachezwa huko Upton Park hapo Aprili 13 kuanzia Saa 3 Usiku, Saa za Bongo.
Timu hizi zilitoka Sare ya 1-1 huko Old Trafford na sasa zimelazimika kurudiana ili kupata Mshindi atakaesonga Nusu Fainali kucheza na Everton Uwanjani Wembley.
Kwenye Nusu Fainali nyingine, ambayo pia itachezwa Wembley, Crystal Palace itaivaa Watford.
TAREHE MUHIMU
Nusu Fainali
Jumamosi 23 Aprili 2016
19:15 Everton v West Ham au Man United
Jumapili 24 Aprili 2016
18:00 Crystal Palace v Watford
Fainali
Jumamosi 21 Mei 2016

No comments:
Post a Comment