Mchezaji Bora wa dunia 2015, Lionel Messi ameeleza hisia zake za sehemu anayopendelea kwenda kucheza soka kabla ya kustaafu kucheza mchezo huo wenye umaarufu mkubwa duniani.
Akizungumza na jarida la El Grafco, Messi alisema kuwa kabla ya kustaafu kucheza soka anapendelea kucheza nchini kwao Argentina na anaamini kuwa uwezekano upo wa kwenda kucheza soka huko.
“Ni jambo ambalo ninalipenda , sijajua lini lakini uwezekano upo,
“Sijapanga itakuwa kwa muda gani kama utakuwa muda mrefu au mfupi lakini ninapenda kuendelea kucheza mwili wangu ukiwa bado unaruhusu na nina kitu naweza kuisaidia timu yangu. Nikijua muda sahihi nitafanya maamuzi,” alisema Messi.
Messi, 28 alianzia maisha yake ya soka kwao Argentina katika klabu ya Newell`s Old Boys ambapo alichukuliwa na kujiunga na kituo cha kukuzia vipaji cha Barcelona (La Masia) mwaka 2001 akiwa na miaka 13.