Tanzia:
Tasnia ya muziki nchini imepata pigo baada ya kupoea kifo cha cha Mzee
Mzee Mapili (Pichani kulia) baada ya kuonekana hajatoka Chumbani kwake
kwa Muda Mrefu…. Ndipo mlango ukavunjwa nyumbani kwake Tabata Matumbi
jijini Dar es salaam na kukuta Mzee wetu hatunaye tena…
Mzee
atakumbukwa kwa Kibao cha “Napenda Nipate Lau Nafasi” na “Rangi Ya
Chungwa” na vingine nyingi…Pia alikuwa kiongozi wa kwanza wa Tanzania
Dance Music Association ama Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania
(CHAMUDATA).
Mara ya mwisho hadharani
Marehemu Mzee Kassim Mapili alionekana akiongoza wanamuziki katika
mazishi ya mwanahabari nguli wa burudani Marehemu Fred Mosha katika
makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam, ambako pamoja na kushirki
mazishi aliimba kwa hisia beti kadhaa za kumuenzi marehemu Fred.MAZISHI YA MZEE KASSIM MAPILI NI LEO IJUMAA 26/02/2016 SAA KUMI JIONI KISUTU. MSIBA UPO MTAA MAGOMENI NA.23 MAPIPA JIJINI DAR ES SALAAM. SHIME TUJITOKEZENI WAPENDWA KUMSINDIKZA MZEE WETU KWENYE SAFARI YAKEYA MISHO.
KAMA UNGEPENDA KUJIUNGA NASI KWA MCHANGO BASI TUMA RAMBIRAMBI KWA HASSAN MSUMARI-KATIBU MKUU CHAMUDATA. NAMBA ZAKE 0717340533 ..
ADDO NOVEMBER – RAIS SHIRIKISHO LA MUZIKI TANZANIA… 0744150000
Imetolewa na Addo November
Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania..!!
No comments:
Post a Comment