Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, January 15, 2016

MTIBWA SUGAR, JKT MGAMBO ZAFANYA MAZOEZI KARUME KUJIANDAA NA MICHEZO YAO YA KESHO

Wachezaji wa Mtibwa Sugar wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Karume leo kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba utakaochezwa Uwanja wa Taifa kesho.

Wachezaji wa JKT Mgambo wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Karume leo kujiandaa na mchezo dhidi ya JKT Ruvu utakaochezwa Uwanja wa Karume kesho.
Wachezaji wa JKT Ruvu wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Karume jana kujiandaa na mchezo dhidi ya JKT Mgambo utakaochezwa Uwanja wa  Karume  kesho.

Baada ya kusimama kwa wiki mbili kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar, Ligi Kuu mzunguko wa kumi na nne (14) unatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo 8 kuchezwa katika viwanja mbalimbali, huku timu 16 zikichuana kusaka pointi 3 muhimu.
Jumamosi Uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, Maafande wa JKT Ruvu watawakaribisha Maafande wa Mgambo Shooting, Toto Africans watawakaribisha Tanzania Prisons Uwanja wa CCM Kirumba, huku Stand United wakicheza dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Uwanja wa Tafa jijini Dar es salaam, Simba SC watawakaribisha wakata miwa wa Mtibwa Sugar saa 10 jioni, Mbeya City watakuwa wenyeji wa Mwadui FC Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Coastal Union dhidi ya Majimaji wanja wa Mkwakwani, huku mchezo kati ya Azam FC dhidi ya African Sports ukianza saa 1 usiku.
Jumapili ligi hiyo itaendelea kwa mchezo mmoja uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, ambapo Young African watawakaribisha Ndanda FC kutoka Mtwara.



No comments:

Post a Comment