Katika kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri,
klabu ya Simba ilianzisha tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kuanzia mwezi
wa Septemba 2015.
Mshindi wa mwezi wa Oktoba, 2015 ni Mohamed Hussen ‘Tshabalala’
ambapo alipigiwa kura nyingi na mashabiki na wapenzi wa Simba na soka
la Tanzania kwa ujumla kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na
huduma ya Simba News.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam Rais wa Simba Evans Aveva
alisema “Uongozi, wanachama na wapenzi wa Simba wanathamini mchango wa
wachezaji katika kuifanya timu yetu ifanye vizuri, hivyo tumeona ni
jambo la busara kuwa klabu ya kwanza nchini Tanzania kuwa na tunzo za
mchezaji wake bora.
“Tunaamini kuwa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa Simba itaongeza ari
na kujituma kwa wachezaji wetu. Sisi tukiwa kama viongozi ni kazi yetu
ya msingi kuhakikisha kuwa wachezaji wetu hasa wale wanaojituma zaidi
wanatambuliwa na kuenziwa’’.
Akizungumza jinsi tuzo ya mchezaji bora itakavyoendeshwa, Imani
Kajula ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa EAG Group ambao ni washauri na
watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba, amesema: “Wanachama na
wapenzi wa Simba na wapenda michezo ndio watakao kuwa wanachagua
mchezaji bora wa mwezi kwa kutuma jina la mchezaji wanayempendekeza
kwenda kwenye namba 15460”.
“Ni wale tu ambao wamejiunga na huduma ya Simba News kupitia mtandao
wa Vodacom na Tigo wataweza kupiga kura kuchagua mchezaji bora wa mwezi
wa Simba’’.
Simba News ni huduma iliyoanzishwa na Simba ili kuwapa wapenzi wa
Simba habari mbalimbali za Simba popote pale walipo ikiwemo matokeo,
majina ya wachezaji wanaocheza mechi, usajili na habari nyingine za
klabu ya Simba.
Kujiunga na Simba News tuma neno Simba kwenda namba 15460 ni maalum kwa wateja wa Tigo na Vodacom pekee.
No comments:
Post a Comment