Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, November 12, 2015

STARS KUJIFUA LEO JIONI TAIFA

Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars’ imerejea jana jioni ikitokea chini Afrika Kusini ilipokuwa imeweka kambi ya siku kumi, ambapo leo jioni itafanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kikosi cha Taifa Stars kinachonolewa na kocha mzalendo Charles Boniface Mkwasa, kimefikia katika hoteli ya Serena iliyopo eneo la Posta, na leo jioni watafanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea klabu ya TP Mazembe ya Congo DR wameungana kambini na wachezaji wenzao jana na kufanya kikosi cha Stars kukamilika kwa maandalizi ya mwisho.
Wapinzani wa Taifa Stars, timu ya Taifa ya Algeria wanatarajiwa kuwasili leo saa 12 jioni nchini kwa usafiri wa ndege binafsi, na kufikia katika hoteli ya Kilimanjaro Kempsink (Hyatt) ambapo kesho jioni Ijumaa watafanya mazoezi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es slaam.
Wakati huo huo waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Mali, mwamuzi wa kati Keita Mahamadou, Diarra Bala, Niare Drissa Kamory na mwamuzi wa akiba Coulibaly Harouna tayari wameshawasili nchini leo asubuhi, huku mtathimini wa waamuzi Attama Ibrahim Boureima kutoka nchini Niger alishawasili nchini tangu juzi usiku.
Kamisaa wa mchezo huo Mukuna Wilfred kutoka nchini Zimbambwe anawasili nchini leo mchana kwa shirika la ndege la Afrika Kusini (South Africa Airways

No comments:

Post a Comment