Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, November 13, 2015

TAIFA STARS KAMILI KUIVAA ALGERIA KESHO



Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ Charles Boniface Mkwasa amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Algeria kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari leo, Mkwasa amesema wamejiandaa kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo, wanajua Algeria ni miongoni mwa timu bora Afrika, lakini hilo halitawazuia kuibuka na ushindi.
“Katika mpira wa sasa duniani hakuna timu kubwa wala timu ndogo, lolote linaweza kutokea, sisi tuna nafasi ya kufanya vizuri tukiwa katika uwanja wa nyumbani na washabiki wetu” alisema Mkwasa.
Aidha Mkwasa alisema wamefanya mazoezi kwa pamoja kwa takribani siku 10, vijana wapo katika hali nzuri, hakuna majeruhi vijana wote wapo katia hali nzuri na timu imefanya mazoezi ya mwisho leo asubuhi kabla ya kushuka dimbani kuwakabili Mbweha wa Jangwani.
Mwisho Mkwasa amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa kuja kuwapa sapoti vijana watakapokuwa wanapeperusha bendera ya Tanzania.
 Mechi kati ya Tanzania dhidi ya Algeria  itaanza saa 10:30 jioni katika uwanja wa Taifa jijini Dares salaam.

No comments:

Post a Comment