TIKETI za mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la
Dunia chini Urusi mwaka 2018 kati ya Tanzania dhidi ya Algeria ziataanza
kuuzwa kesho Ijumaa katika vituo 10 viliyopo jijini Dar es salaam.
Magari
maalumu yenye stika yataanza kuuza tiketi hizo za mchezo kesho saa 2
kamili asubuhi mpaka saa 12 jioni, ambapo tiketi zinauzwa kwa shilingi
elfu tano (5,000) kwa viti vya rangi ya bluu na kijani na rangi ya
machungwa, na elfu kumi (10,000) kwa viti vya VIP B & C.
Vituo
vitakavyotumika kuuza tiketi hizo ni ofisi za TFF – Karume, Buguruni –
Oilcom, Mbagala – Darlive, Mnazi Mmoja, Luther House – Posta, Big Bone –
Msimbazi, Ubungo – Oilcom, Makumbusho – Stand ya Daladala, Uwanja wa
Uhuru.
TFF inawaomba wadau, washabiki na watanzania
kujitokeza kwa wingi kununua tiketi za mchezo huo katika magari maalumu
yatakayokuwepo kwenye vituo vilivyotajwa, ili kuondokana na tatizo la
kuuziwa tiketi zisizokuwa halali.
Wakati huo huo
Ubalozi wa Algeria nchini Tanzania, umewataka waandishi wa habari
wanaotrajia kwenda kuripoti mchezo wa marudiano jijini Algiers siku ya
jumanne, kuwasilisha maelezo ya chombo wanachofanyia kazi pamoja na
vifaa watakavyovitumia kwenye mchezo huo (camera, vinasa sauti)
kuwasilisha maelezo hayo leo Alhamsi kabla ya saa 9 mchana katika ofisi
za Ubalozi huo kwa ajili ya kupatiwa Accreditation za kufanyia kazi.
Matokeo ya mchezo wa jana Azam Sports Federtaion Cup (ASFC), ni Mshikamano 0 - 1 Cosmopolitan
No comments:
Post a Comment