Stars inahitaji sare ya kuanzia mabao 3 au kupata ushindi wa aina yoyote ugenini dhidi ya Msumbiji maarufu kama Mambas |
Msafara wa watu 27 wa kikosi cha
timu ya Taifa (Taifa Stars) kinaondoka kesho (Julai 30 mwaka huu) saa 10 jioni
kwa ndege ya Air Tanzania kwenda Afrika Kusini ambapo kitapiga kambi ya siku
mbili kabla ya kuingia Maputo kuikabili Msumbiji (Mambas).
Taarifa
ya afisa habari na mawasiliano wa shirikisho la soka nchini Tanzania
Bonface Wambura imesema timu hiyo itawasili saa 9 asubuhi kesho (Julai
30 mwaka huu)
kwa ndege ya Fastjet kutoka Tukuyu mkoani Mbeya, na baadaye jioni
kuunganisha
safari ya Afrika Kusini.
Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya
pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji itachezwa Agosti 3 mwaka huu
Uwanja wa Taifa uliopo Zimpeto nje kidogo ya Jiji la Maputo.
Msafara huo wa Taifa Stars kwenda
Afrika Kusini unajumuisha wachezaji 19 na waliobaki ni maofisa wa Benchi la
Ufundi lililo chini ya Kocha Mkuu Mart Nooij kutoka Uholanzi.
Wakati kiungo Mwinyi Kazimoto
ametua leo (Julai 29 mwaka huu) nchini kuungana na wenzake, washambuliaji
Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wao wataungana na wenzao kesho (Julai 30
mwaka huu) jijini Johannesburg wakitokea Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo (DRC).
Wakati huo huo, Serengeti Boys
imewasili salama jana (Julai 28 mwaka huu) jijini Johannesburg kwa ajili ya
mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka
17 dhidi ya wenyeji Afrika Kusini (Amajimbos).
Serengeti Boys imefikia hoteli ya
Garden Court, na mechi hiyo itachezwa Jumamosi (Agosti 2 mwaka huu) kwenye
Uwanja wa Dobsonville uliopo Soweto. Timu hizo zilitoka suluhu katika mechi ya
kwanza iliyochezwa karibu wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment