Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amefunguliwa mashitaka na FA, Chama cha Soka England, kwa utovu wa nidhamu.
Maneno ambayo yanaweza kumsulubu Mourinho yalitolewa Jumamosi mara baada ya Chelsea kuchapwa 3-1 na Southampton kwenye Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Uwanjani Stamford Bridge.
FA imedai maneno ya Mourinho yanamaanisha Marefa wanapendelea na hivyo ni kinyume cha Sheria.
Kwenye Mechi hiyo na Southampton Mourinho alichukizwa na Refa Robert Madley kuwanyima Penati na kudai Marefa huogopa kuwapa Chelsea Penati.
Mourinho, mwenye Miaka 52, amepewa hadi Alhamisi Oktoba 8 Saa 2 Usiku kwa Saa za Tanzania, kujibu mashitaka hayo.
Hiyo Jumamosi, mara baada ya kutoa kauli yake, Mourinho pia alitabiri FA itamfungulia mashitaka.
Licha ya kusakamwa na vipigo Vinne katika Mechi 8 za Ligi Kuu England ambayo wao ndio Mabingwa na kutupwa Nafasi ya 16 wakiwa Pointi 10 nyuma ya Vinara Man City, Klabu ya Chelsea Jana ilisema bado wana imani na Mourinho.
No comments:
Post a Comment