Kocha wa Simba Dylan Kerr akimkabidhi Hamisi Kiiza Tunzo ambayo ni zawadi ya mchezaji bora wa Simba wa Septemba |
MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Simba, Hamis Kiiza amekuwa mchezaji wa kwanza kupata tunzo ya mchezaji bora wa Septemba wa tunzo zilizoanzishwa na uongozi wa Simba.
Kiiza amepewa 500,000 na kukabidhiwa na kocha Dylan Kerr na kusema ni wakati wa wachezaji kuonesha ushindani mkubwa kwani uongozi umekuja na wazo zuri la kutoa mchezaji bora kila mwezi”, alisema Kerr
“Kila mtu ana uwezo lakini kuwa mchezaji bora ni kufanya mazoezi, nidhamu ya mchezo ukiwa uwanjani na hata nje ya uwanja na kujituma hapo unaweza kuwa mchezaji bora wa mwezi”, alisema Kerr
Naye Rais wa Simba, Evans Aveva alisema uongozi, wanachama na wapenzi wa Simba wanathamini mno mchango wa wachezaji katika kuifanya timu yao ifanye vizuri, hivyo wameona ni jambo la busara kuwa klabu ya kwanza Tanzania kuwa na tunzo za mchezaji wake bora.
“Tunaamini kuwa tunzo ya mchezaji bora wa mwezi wa Simba itaongeza ari na kujituma kwa wachezaji wetu hivyo tukiwa kama viongozi ni kazi yetu ya msingi kuhakikisha kuwa wachezaji wetu hasa wale wanaojituma zaidi wanatambuliwa na kuenziwa”, alisema Aveva
Mchezaji bora wa mwezi anapatikana kwa kutuma jina la mchezaji wanayempendekeza kwenda kwenye namba 15460, ni wale tu ambao wamejiunga na Simba News kupitia mtandao wa Vodacom na Tigo wataweza kupiga kura kuchagua mchezaji bora wa mwezi wa Simba’’
Zoezi la kumchagua mchezaji bora wa mwezi wa Octoba, 2015 linaanza Octoba 10. Piga kura mara nyingi zaidi kuweza kumpata mchezaji wako bora wa Octoba.
Simba News ni huduma iliyoanzishwa na Simba ili kuwapa wapenzi wa Simba habari mbalimbali za Simba popote pale walipo ikiwemo matokeo, majina ya wachezaji wanaocheza mechi, usajili na habari nyingine za klabu ya Simba.
Kujiunga na Simba News tuma neno Simba kwenda namba 15460 ni maalum kwa Tigo na Vodacom.
No comments:
Post a Comment