KATIKA kuzipa
pengo la beki Mghana, Joseph Zuttah ‘Teteh’Yanga imemsajili beki wa kati Vicncent Bossou ambaye pia ni mchezaji wa timu ya
taifa ya Togo.
Tayari Bossou yuko nchini na inaonekana lazima
atajiunga na Yanga ambayo inataka kuimarisha safu ya ulinzi ambayo ilionekana
imepwaya wakati ikishiriki mashindano ya Kagame na kuondolewa kwenye hatua ya
robo fainali.
Beki huyo alianza soka lake kwenye klabu ya
Maranatha FC mwaka 2006 na kudumu kwenye klabu hiyo mpaka mwaka 2009 akicheza
jumla ya mechi 77 na kuifungia klabu hiyo magoli matano.
Alijiunga na klabu ya Etoile Sportive du
Sahel, Januari 2010 kwa mkataba wa miaka miwili lakini mkataba wake ukavunjwa
baada ya miezi mitatu baadae akiwa ameichezea klabu hiyo mechi tatu tu, na karudi
tena Maranatha FC Machi 18, 2010.
Mei 2011 alijiunga na klabu ya Navibank
Saigon F.C ya Vietnam ambapo alicheza mechi 35 na kufanikiwa kufunga mabao
matatu na kwa sasa alikuwa na mkataba na klabu ya Govang Hi FC ya Korea
Kusini.
Pia Bossou alikuwepo kwenye kikosi cha Togo
ambacho kilijitoa kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika 2010 baada ya basi la
timu hiyo kushambuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni magaidi wakati waelekea nchini
Angola ambako ndipo mahindano yalikuwa yafanyik.
Ameshaichezea timu ya taifa ya Togo kwenye
michezo 25, hajafanikiwa kufunga goli hata moja kwa mechi zote alizocheza.
Vincent Bossou alizaliwa Februari 7, 1986 kwenye mji wa Kara, Togo
ana urefu mita
1.86 sawa na futi 6 na inchi moja.
Yanga wamemsajili beki huyo kwa ajili ya kuiongezea
nguvu safu yao ya ulinzi ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikitumikiwa na mabeki
wawili Nadir Haroub ‘Canavaro’ na Kelvin Yondani ambao ubora wao unapungua
kutokana na kucheza mechi nyingi bila kupumzika.
Ikumbukwe kuwa Yanga wataiwakilisha Tanzania kwenye
michuano ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika hivyo wanahitaji kuwa na wachezaji
wenye ubora wa kupambana kwenye michuano hiyo.
Wakati Bossou anachukua nafasi ya Teteh, kiungo
Mzimbabwe, Thaban Kamusoko yeye anajiunga na Yanga na kuchukua nafasi ya Kpah
Sherman.
Sherman tayari amejiunga na kikosi cha Mpumalanga
Black Aces cha nchini Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment