BAADA ya
Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) kumweka huru aliyekuwa
golikipa wa Yanga Juma Kaseja
klabu za Mbeya City, Mwadui FC na Ndanda FC zinapigana vikumbo kuwania
saini yake.
Akizungumza jijini Kaseja amekiri
kufutwa na viongozi wa klabu hizo lakini hakuweka wazi ni klabu gani ambayo
atajiunga nayo akitaka mashabiki wasubiri watajua muda ukifika.
“Ni kweli nimefanya
mazungumzo na viongozi wa Mbeya City kwa ajili ya kunisajili na naamini Mbeya
City ni timu nzuri ambayo inaleta changamoto pia kocha wao Juma Mwambusi
tunafahamaana tangu akifundisha Moro Utd, na leo (jana) timu ya Ndanda ya
mkoani Mtwara imeonyesha nia ya kunisajili hivyo tunavyozungumza wakala wangu
yupo nao kwenye mazungumzo”, alisema Kaseja.
Kocha wa Mwadui
FC, Jamhuri Kihwelo amekaririwa na vyombo vya habari akisema endapo mambo
yatakwenda vizuri atamsajili Kaseja kwani ni kati ya magolikipa npra nchini.
Aidha Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa amethibitisha kumruhusu Kaseja kujiunga na klabu yoyote ambayo atakubaliana nayo atacheza kwa muda wote ambao suala lake la mgogoro na Yanga likiwa linashughulikiwa kwani hawajamwondoa kwenye mgogoro wa kikazi na klabu yake.
No comments:
Post a Comment