WAKATI
awali dirisha la usajili wa ligi lilikuwa lifungwe jana saa sita usiku, Shirikisho la Mpira wa Miguu
nchini (TFF) limesogezwa mbele mpaka Agosti 20 mwaka huu.
Akizungumza
na wandishi wa habari, Afisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto alisema dirisha la
usajili wa wachezaji kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na
Ligi Daraja la Pili (SDL) sasa litafungwa
Agosti 20 mwaka huu.
“Awali dirisha la usajili lilikua lifungwe leo (jana), na
usajili mdogo wa ndani ungefungwa Septemba 5, 2015 lakini sasa usajili wote kwa
jumla utafungwa Agosti 20”, alisema Kizuguto.
Pia
alisema Agosti Agosti 21- 28 ni kipindi
cha pingamizi, Agosti 29-30 ,Kamati ya
Sheria na Hadhi za Wachezaji itapitia na kupitisha usajili.
Dirisha
la uhamisho wa wachezaji wa Kimataifa (FIFA –TMS) litafungwa Septemba, 6 na
Ligi Kuu inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 12.
Aidha
TFF inavitaka vilabu kukamilisha usajili huo katika muda uliowekwa, ili
kupunguza usumbufu wa kufanya usajili dakika za mwisho,na dirisha
litakapofungwa Agosti 20, litafunguliwa tena wakati wa dirisha dogo mwezi
Novemba 15 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment