BAADA ya kuisaidia timu yake ya Azam FC kutwaa kombe
la Kagame 2015, Farid Mussa pamoja na wachezaji wenzake nane wameitwa kwenye
kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ chenye wachezaji 29 kitakachocheza na
Nigeria.
Awali akitangaza kikosi hicho ambacho kitaingia
kambini jumapili, Kocha
Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface, aliweka wazi
kuwa wameangalia wachezaji kwenye mashindano ya Kagame, ambayo yamemalizika
hivi karibuni.
“Kikosi
hiki cha wachezaji 29 wataingia kambini siku ya Jumapili katika hoteli ya
Tansoma iliyopo Gerezani kwa ajili ya kambi ya wiki moja ya mazoezi kabla ya
kwenda kuweka kambi ya siku kumi jijini Istambul - Uturuki, ambapo itacheza
michezo miwili ya kirafiki na timu za Taifa za Libya na Kuwait kabla ya kurejea
nchini kuwavaa Nigeria”, alisema Mkwassa
Katika
kikosi hicho Mkwasa amewajumuisha wachezaji watano wanaocheza soka la kulipwa
nje ya nchi (Proffesional), ambao baadae watajumuika kwa kambi ya kujiandaa
kucheza na Nigeria, Septemba 2015 nchini Uturuki.
Katika
kikosi hicho klabu ya ndio imeongoza kutoa wachezaji wengi, ambapo Azam FC
wachezaji tisa, Yanga wachezaji ni saba, Simba wameitwa wachezaji watatu huku
Mwadui FC, Ruvu Shooting na Mafunzo zikiwatoa mchezaji mmoja mmoja.
Wachezaji
walioitwa ni magolikipa, Ally Mustafa (Yanga SC) na Aishi Manula (Azam FC),
walinzi wa pembeni: Shomari Kapombe (Azam FC), Michael Aidan (Ruvu Shooting),
Juma Abdul, Mwinyi Haji (Yanga SC) na Abdi Banda (Simba SC).
Walinzi
wa kati; Hassan Isihaka (Simba SC), Nadir Haroub, Kelvin Yondani (Yanga SC),
Viungo wakabaji: Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya (Azam FC), Viungo
washambuliaji ni Salum Telela (Yanga SC) na Said Ndemla (Simba SC).
Washambuliaji
wa pembeni; Orgenes Mollel (Aspire – Senegal), Abdrahman Mbambi (Mafunzo), Deus
Kaseke, Saimon Msuva (Yanga SC), Ramdhani Singano, Farid Musa (Azam FC), huku
washambuliaji wa kati wakiwa ni John Bocco, Ame Ally (Azam FC) na Rashid
Mandawa (Mwadui FC).
Wachezaji
wa kimataifa waliojumuishwa katika kikosi hicho ambacho Agosti 23 kitaelekea
kambini nchini Uturuki kwa kambi ya siku kumi ni Mbwana Samata, Thomas
Ulimwengu (TP Mazembe – DR Congo), Mrisho Ngasa (Free State - Afrika Kusini) na
Hassan Sembi (Santos FC – Afrika Kusini) na Adi Yussuf (Mansfield Town – Uingereza
No comments:
Post a Comment