Timu
ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) inatarajiwa kuingia kambini
kesho kisiwani Zanzibar kujiandaa na Fainali za Michezo ya Afrika (All Africa
Games) zitakazofayika mwezi Septemba mwaka huu nchini Congo Brazzavile.
Kikosi
hicho cha wachezaji 25 chini ya Kocha Mkuu Rogasian Kaijage, tayari kimeanza
mazoezi kujiandaa na michuano hiyo ambapo Tanzania ilikata tiketi ya kushiriki
fainali hizo baada ya kuiondoa Zambia kwa jumla ya mabao 6-5.
Twiga
Stars inaingia kambini kwa gharama za
TFF, huku jitihada za TFF kuwasiliana na Kamati ya Olimpiki nchini (TOC)
zikiendelea kuona ni jinsi gani kamati hiyo inaihudumia timu hiyo ya Taifa kwa
ajili ya maandalizi ya michuano hiyo ya Michezo Afrika.
TFF
inatambua TOC ndio wana jukumu la kuhudumia timu za Taifa kuelekea kwenye
michuano hiyo ya Michezo ya Afrika ikiwemo Twiga Stars.
Twiga
Stars ambayo imefuzu kwa Fainali za Michezo ya Afrika itakayoanza kutimua vumbi
Septemba 04 – 17 imepangwa kundi A na wenyeji Congo Brazaville na Nigeria
pamoja na Ivory Coast.
No comments:
Post a Comment