TIMU ya Olympiki maalumu
ambayo ilikuwa inashiriki mashindano ya dunia nchini Marekani inamewasili leo
saa 9.15 alasiri kwa ndege ya Emirates.
Akizungumza
baada ya kuwasili, Mkuu wa Msafara wa timu hiyo, Frank Macha, alisema
anashukuru kurudi salama na mafanikio walioyopata kwani wamefanya vizuri.
“Timu
yetu imefanya vizuri kwani timu ina wachezaji wanane na imepata medali kumi,
dhahabu tatu, fedha nne na shaba tatu”, alisema Macha.
Michezo
hiyo ilifunguliwa Julai 25 na ilifungwa Agosti 2 huku Tanzania ikiwakilishwa na
wachezaji wanane, wasichana wanne na wavulana wanne wa mchezo wa riadha baada
ya kukosekana pesa za kupeleka timu ya soka.
Michezo
ambayo walipata medali ni mbio za mita 100, mita 200, mita 400, mita 800 na
mita 5000.
Mbio za kupokezana vijiti (4 x 100) iliambulia nafasi ya nne na hivyo
hawakupata medali.
No comments:
Post a Comment